Deuteronomy 5:1-6

Amri Kumi

(Kutoka 20:1-17)

1 aMusa akawaita Israeli wote, akawaambia:

Ee Israeli, sikilizeni amri na sheria ninazowatangazia leo. Jifunzeni, na mwe na hakika kuzifuata.
2 b Bwana Mwenyezi Mungu wetu alifanya Agano nasi katika mlima wa Horebu. 3 cSi kwamba Bwana alifanya Agano na baba zetu, bali alifanya nasi, nasi sote ambao tuko hai hapa leo. 4 d Bwana alisema nanyi uso kwa uso kutoka moto juu ya mlima. 5 e(Wakati huo nilisimama kati ya Bwana na ninyi kuwatangazia neno la Bwana, kwa sababu mliogopa ule moto, nanyi hamkupanda mlimani.) Naye Mungu alisema:

6 f“Mimi ndimi Bwana Mwenyezi Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, kutoka nchi ya utumwa.
Copyright information for SwhKC